Matthew 27:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wewe! Si ulijidai kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi, shuka msalabani!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka msalabani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kwa kusema, “Ulisema ungeweza kubomoa Hekalu na kulijenga tena katika siku tatu. Jiokoe mwenyewe! Teremka chini kutoka kwenye huo msalaba ikiwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wewe! Si ulijidai kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi, shuka msalabani!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka msalabani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka kutoka msalabani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wewe! Si ulijidai kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi, shuka msalabani!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakisema: Wewe unayelivunja Jumba la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe! Ukiwa Mwana wa Mungu shuka msalabani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakisema: “Wewe uliyetaka kubomoa hekalu na kujenga lingine katika siku tatu, ujiokoe sasa wewe mwenyewe! Kama wewe ni Mwana wa Mungu, ujishushe juu ya musalaba!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakinena, Ewe ulivunjae hekalu na kuijenga kwa siku tatu, jiponye nafsi yako; ukiwa Mwana wa Mungu, shuka msalahani.