Matthew 27:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Ati yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni mfalme wa Israeli! Ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa yeye mwenyewe! Watu husema kuwa yeye ni mfalme wa Israeli. Ikiwa yeye ni mfalme, ashuke kutoka msalabani. Ndipo tutamwamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Ati yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni Mfalme wa Israeli! Ashuke sasa kutoka msalabani, tutamwamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni Mfalme wa Israeli! Ashuke sasa kutoka msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Ati yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wengine aliwaokoa, lakini mwenyewe hawezi kujiokoa. Kama ndiye mfalme wa Waisiraeli, ashuke sasa hivi msalabani! Ndivyo, tutakavyomtegemea nasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Aliokoa wengine, lakini sasa anashindwa kwa kujiokoa yeye mwenyewe! Yeye ni mufalme wa Waisraeli, sasa ajishushe pale juu ya musalaba kusudi nasi tupate kumwamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Aliponya watu wengine, hawezi kujiponya nafsi yake. Akiwa mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani, naswi tutamwamini.