Matthew 27:54 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa sana, wakapaza sauti na kusema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Afisa wa jeshi na askari waliokuwa wanamlinda Yesu walitetemeka sana kwa kuogopa tetemeko la ardhi na kila walichokiona kikitokea. Wakasema, “Hakika alikuwa Mwana wa Mungu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, wakaogopa wakasema, “Hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa, wakasema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini bwana askari nao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoliona lile tetemeko na yale mambo yaliyokuwapo, wakaogopa sana, wakasema: Kweli, huyu alikuwa Mwana wa Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukubwa wa waaskari na wale waliokuwa pamoja naye wakimuchunga Yesu walipoona tetemeko la inchi na mambo yote yaliyofanyika, wakaogopa sana, na kusema: “Hakika mutu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.