Matthew 27:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viongozi wa makuhani wakaviokota vile vipande vya fedha Hekaluni. Wakasema, “Sheria yetu haituruhusu kuweka fedha hii katika hazina ya Hekalu, kwa sababu fedha hii imelipwa kwa ajili ya kifo, ni fedha yenye damu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, “Haifai kuziweka katika hazina ya hekalu kwa maana ni fedha za damu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watambikaji wakuu wakaziokota zile fedha, wakasema: Ni mwiko kuzitia katiaka sanduku ya vipaji, kwa kuwa ni fedha za damu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wa makuhani wakaokota zile feza na kusema: “Kufuatana na Sheria yetu hairuhusiwi kuweka feza kama hizi ndani ya sanduku ya hekalu kwa sababu feza hizi ni za damu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makuhani wakuu wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Ni haramu kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu.