Matthew 27:60 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yusufu akauzika mwili wa Yesu katika kaburi mpya alilokuwa amelichonga kwenye mwamba mlimani. Kisha akalifunga kaburi kwa kuvingirisha jiwe kubwa kuziba mlango wa kaburi. Baada ya kufanya hivi, akaondoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kuuzika kwenye kaburi lake mwenyewe jipya alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mlangoni mwa kaburi, akaenda zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani. Akafingirisha jiwe kubwa mlangoni pa kaburi, akaenda zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaiweka ndani ya kaburi lake jipya alilojichimbia katika jiwe. Kisha akasukumia jiwe kubwa kwenye kiingilio cha lile kaburi na kujiendea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akanweka katika kaburi lake jipya, alilolikata mwambani; akafingirisha jiwe kubwa hatta mlango wa kaburi, akaenda zake.