Matthew 28:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanawake wakiwa njiani wakienda, baadhi ya wale askari waliokuwa wakilinda kaburi walienda mjini na kuwaeleza viongozi wa makuhani kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanawake wakaenda kuwaambia wafuasi. Na wakati huo huo baadhi ya askari waliokuwa wanalinda kaburi waliingia mjini. Walikwenda kuwaambia viongozi wa makuhani kila kitu kilichotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wale wanawake wakiwa njiani wakienda, baadhi ya wale askari waliokuwa wakilinda kaburi walienda mjini na kuwaeleza viongozi wa makuhani kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wale wanawake walikuwa njiani wakienda, baadhi ya wale askari waliokuwa wakilinda kaburi walienda mjini na kuwaeleza viongozi wa makuhani kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya walinzi waliingia mjini, wakawaambia wakuu wa makuhani juu ya mambo yote yaliyotendeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanawake walipokuwa wanakwenda zao, baadhi ya walinzi wa lile kaburi walikwenda mjini kutoa taarifa kwa makuhani wakuu juu ya mambo yote yaliyotukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwenda zao, mara nao walinzi wakafika mjini mmoja mmoja, wakasimulia watambikaji wakuu yote yaliyokuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanawake walipokuwa wakienda, waaskari wamoja kati ya wale waliochunga kaburi wakaenda katika muji na kuwapasha wakubwa wa makuhani habari za mambo yote yaliyotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao walipokuwa wakienda njiani, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha makuhani wakuu khabari za mambo yote yaliyotendeka.