Matthew 28:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagizia Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Isa alikuwa amewaagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale wafuasi kumi na mmoja walikwenda Galilaya, kwenye mlima ambao Yesu aliwaambia waende.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagiza Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagizia Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Yesu alikuwa amewaagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Isa alikuwa amewaagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya hadi katika mlima ule aliowaagiza Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanafunzi kumi na mmoja walikwenda Galilaya kwenye ule mlima aliowaagizia Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilea, wakafika mlimani pale, Yesu alipowaagizia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wale wanafunzi kumi na mumoja wakaenda Galilaya kwa mulima ule Yesu aliowaagiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale wanafunzi edashara wakaenda Galilaya hatta mlima ule aliowaagiza Yesu.