Matthew 28:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghafla kukatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula, pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Mwenyezi Mungu alishuka kutoka mbinguni, akaenda kwenye kaburi, akalivingirisha lile jiwe na kulikalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ghafla malaika wa Bwana akaja kutoka mbinguni, na tetemeko kubwa likatokea. Malaika alikwenda kaburini na kulivingirisha jiwe kutoka kwenye mlango wa kaburi. Kisha akaketi juu ya jiwe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ghafla kutatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghafla kukatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni akaenda penye kaburi akalivingirisha lile jiwe na kulikalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula, pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Mwenyezi Mungu alishuka kutoka mbinguni, akaenda penye kaburi, akalivingirisha lile jiwe na kulikalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghafla kukatokea tetemeko kubwa la nchi; malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akalivingirisha lile jiwe, akalikalia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara kukawa na tetemeko kubwa la nchi. Kwani malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akaja akalifingirisha lile jiwe, likatoka mlangoni, akalikalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa rafla kukatokea tetemeko la inchi, kwa maana malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akasukuma lile jiwe lililofunga kaburi pembeni na kuikaa juu yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake.