Matthew 28:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hayupo hapa. Amefufuka kutoka kwa wafu, kama alivyosema. Njooni mwone mahali ulipokuwa mwili wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njoni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama vile alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hayupo hapa; maana amefufuka kama alivyosema. Njooni, mpatazame mahali alipolazwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hayupo hapa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni mkaone mahali alipokuwa amelala.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayumo humu, kwani amefufuliwa, kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali, Bwana alipokuwa amewekwa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye hayuko hapa: amefufuka sawa alivyosema. Mukuje, muone pahali walipolalisha maiti yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana.