Matthew 28:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka kwa wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu, naye anawatangulia kwenda Galilaya. Mtamwona huko.’ Sasa nimekwisha kuwaambia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nendeni haraka mkawaambie wafuasi wake, ‘Yesu amefufuka kutoka kwa wafu. Amekwenda Galilaya na atafika huko kabla yenu. Na mtamwona huko.’” Kisha malaika akasema, “Sasa nimewaambia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka kwa wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu, naye awatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtakakomwona. Sasa nimekwisha kuwaambia.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu, naye awatangulia kwenda Galilaya. Huko ndiko mtamwona. Sasa nimekwisha kuwaambia.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba amefufuka kutoka kwa wafu, na sasa anawatangulieni kule Galilaya; huko mtamwona. Haya, mimi nimekwisha waambieni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi nendeni upesi, mwaambie wanafunzi wake kwamba: Amefufuliwa katika wafu! Tazameni, anawatangulia ninyi kwenda Galilea. Huko ndiko, mtakakomwona. Tazameni, nimekwisha kuwaambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muende upesi kuwaambia wanafunzi wake kwamba amefufuka, naye anawatangulia Galilaya, ni kule watakapomwona. Basi, nimekwisha kuwaambia ninyi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Shikeni njia upesi, kawaambieni wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu; Tazama, anatangulia mbele yenu kwenda Galilaya; huko mtamwona: haya, nimewaambieni.