Matthew 28:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini wakiwa wamejawa na hofu, lakini wakiwa na furaha nyingi. Wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo wanawake wakaondoka haraka kaburini. Waliogopa sana, lakini walijawa na furaha. Walipokuwa wanakimbia kwenda kuwaambia wafuasi wake kilichotokea,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini, wakiwa wamejawa na hofu lakini wenye furaha nyingi, wakaenda mbio ili kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini wakiwa wamejawa na hofu, bali wakiwa na furaha nyingi. Wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakiwa wenye hofu na furaha kubwa, hao wanawake walitoka upesi kaburini, wakakimbia kwenda kuwaambia wanafunzi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakatoka upesi kaburini wakishikwa na woga, tena wakifurahi sana, wakaenda mbio kuwasimulia wanafunzi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wale wanawake wakaondoka upesi kutoka kwenye kaburi, wakijazwa na woga na furaha kubwa vilevile. Wakakimbia kwenda kuwapasha wanafunzi wake habari ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.