Matthew 28:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula, Isa akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
ghafla Yesu alisimama mbele yao. Akasema, “Salamu!” Wanawake wakamwendea wakamshika miguu na wakamwabudu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara, Yesu akakutana nao, akawasalimu: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula Yesu akakutana nao, akasema, “salamu!” Wale wanawake wakamkaribia wakaishika miguu yake, wakamwabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula, Isa akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara, Yesu akakutana nao, akasema: “Salamu.” Hao wanawake wakamwendea, wakapiga magoti mbele yake, wakashika miguu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara Yesu akakutana nao, akasema: Salamu kwenu! Nao wakamjia, wakamshika miguu yake, wakamwangukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja Yesu akakutana na wale wanawake, akawasalimia. Wakajongea karibu naye, wakamushika miguu na kumwabudu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.