Matthew 3:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye atakuja akiwa tayari kwa ajili ya kuisafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri kutoka kwenye makapi, na kisha ataiweka nafaka nzuri kwenye ghala yake. Kisha atayachoma makapi kwa moto usiozimika.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Chombo chake cha kupuria kiko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, akiikusanya ngano yake ghalani na kuyachoma makapi kwa moto usiozimika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ungo wa kupepetea umo mkononi mwake, naye atapafagia pake pa kupuria ngano. Ngano zake atazikusanya, aziweke chanjani, lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye anashika lungo katika mikono yake kwa kupepeta ngano. Atakusanya ngano na kuitia katika gala yake, lakini atateketeza maganda katika moto usiozimika.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.