Matthew 3:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninajua mnachofikiri. Mnataka akasema kuwa, ‘lakini Ibrahimu ni baba yetu!’ Hiyo haijalishi. Ninawaambia Mungu anaweza kumzalia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe haya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, Baba yetu ni Abrahamu! Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala msidhani mnaweza kusemezana, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka katika mawe haya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msiwaze mioyoni mwenu kusema: Tunaye baba yetu, ndiye Aburahamu! Kwani nawaambiani: katika mawe haya ndimo, Mungu awezamo kumwinulia Aburahamu wana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musijifikiri kwamba munaweza kujidai tu kuwa Abrahamu ndiye babu yenu. Ninawaambia kwamba Mungu anaweza kugeuza mawe haya kuwa watoto wa Abrahamu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.