Matthew 4:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa walikuwa wavuvi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa maana wao walikuwa wavuvi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Yesu alipokuwa akitembea kandokando ya bahari ya Galilea akaona watu wawili waliokuwa ndugu, ni Simoni aitwaye Petero na nduguye, Anderea. Aliwaona, wakitupa nyavu zao baharini, kwani walikuwa wavuvi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa akitembea pembeni ya ziwa la Galilaya, akawaona wavuvi wawili, waliokuwa wandugu wa tumbo, Simoni (aliyeitwa Petro) na ndugu yake Andrea. Walikuwa wakitupa nyavu katika ziwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi.