Matthew 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa mara nyingine, ibilisi akampeleka Isa hadi kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonesha falme zote za dunia na fahari zake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Isa mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Msengenyaji akampeleka, akampandisha mlima mrefu sana, akamwonyesha ufalme wote pia wa ulimwengu huu na utukufu wake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Shetani akamupeleka tena mpaka juu ya mulima murefu, akamwonyesha falme zote za dunia na utajiri wao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia,