Matthew 5:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu chochote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yo yote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu chochote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ninyi m chumvi ya nchi. Lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi, itatiwa kitu gani, ipate kukolea tena? Hakuna kitu tena, ilichokifalia, itatupwa tu nje, ikanyagwe na watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ninyi ni kama chumvi kwa watu wote. Lakini kama chumvi ikipoteza onjo lake, itatiwa nini ipate tena kukolea? Haifai tena hata kidogo, inabakilia kutupwa na kukanyagwa na watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.