Matthew 5:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliye ndani ya ile nyumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawawashi taa na kuificha kwenye chungu. Bali huiweka kwenye kinara cha taa ili nuru iangaze kwa kila mtu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watu wakiwasha taa hawaiweki chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango; ndivyo inavyowaangazia wote waliomo nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mutu anayewakisha taa na kuiweka chini ya kitunga, lakini anaiweka juu ya kinara kusudi iwaangazie wote wanaokuwa ndani ya nyumba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani.