Matthew 5:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana, amin nawaambia, hadi mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwa Torati, hadi kila kitu kiwe kimetimia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, amin,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Torati, mpaka kila kitu kiwe kimetimia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nawaambiani: Mpaka hapo, mbingu na nchi zitakapokoma, hata kiandiko kimoja au kichoro kimoja kilichomo katika Maonyo hakitakoma, isipokuwa yametimizwa yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli ninawaambia: kwa muda wote mbingu na dunia vitakapokuwa vingali, hakuna hata herufi moja wala nukta moja ya Sheria itakayoondoshwa mpaka yote yatimie.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.