Matthew 5:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Patana na mshtaki wako upesi wakati mpo njiani kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akiwepo mtu anayetaka kukushtaki, patana naye haraka. Jitahidi kufanya hivyo kabla ya kufika mahakamani, hata kama bado mpo njiani. Usipofanya hivyo anaweza kukupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakupeleka kwa walinzi watakaokufunga gerezani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umwitikie mshtaki wako upesi ukiwa naye, mngaliko njiani! Maana mshtaki wako asikupeleke kwa mwenye hukumu, naye mwenye hukumu asikutie mkononi mwa askari, ukatiwa kifungoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kama mutu akikushitaki, upatane naye upesi wakati mungali katika njia kwenda kwenye tribinali. Kama si vile, yule anayekushitaki atakutoa kwa mwamuzi, naye mwamuzi atakupeleka kwa askari, nawe utatupwa katika kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja nae njiani; yule mshtaki asije akakupeleka kwa kadhi, kadhi akakutia mkononi mwa askari, ukatupwa kifungoni.