Matthew 5:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninawaambia kuwa, kila atakayemtaliki mkewe kutokana na sababu isiyohusiana na uzinzi, anamfanya mke wake kuwa mzinzi. Na kila atakayemwoa mwanamke aliyetalikiwa, atakuwa anazini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mtu akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mimi nawaambia, ye yote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na ye yote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa azini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi nawaambiani: kila mtu anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa ajili ya ugoni, huyo anamzinisha. Naye atakayeoa mke aliyeachwa anazini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mimi ninawaambia: mutu yeyote anayeachana na muke wake, isipokuwa tu kwa sababu ya uzinzi, anamufanya muke yule kuwa muzinzi kama akiolewa tena. Na mutu anayemwoa yule muke aliyefukuzwa, anazini vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali mimi nawaambieni, Killa mtu amwachae mkewe, isipokuwa kwa khabari ya asharati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.