Matthew 5:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Mwenyezi Mungu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, mmesikia hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Unaweka kiapo, usishindwe kutimiza kile ulichoapa kufanya. Timiza kiapo ulichoweka mbele za Bwana.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Tena mmesikia kuwa watu wa kale waliambiwa: Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana Mwenyezi Mungu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mmesikia, ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiape kiapo cha uwongo, lakini umtimizie Mungu, uliyomwapia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mumesikia vilevile kwamba babu zenu waliambiwa hivi: ‘Usifanye viapo vya uongo, lakini sherti utimize viapo vyako mbele ya Bwana.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usifanye zuli, bali mtimizie Bwana nyapo zako;