Matthew 5:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sema ‘ndiyo’ tu kama una maana ya ndiyo na ‘hapana’ tu kama una maana ya hapana. Ukisema zaidi ya hivyo, utakuwa unatoa kwa Yule Mwovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ukisema, Ndiyo, basi iwe Ndiyo; ukisema Siyo, basi iwe kweli Siyo. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Ndiyo,’ yenu iwe ‘Ndiyo’ na ‘Hapana’, yenu iwe ‘Hapana.’ Lo lote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli! Au mkisema: Sio, iwe sio kweli! Lakini yanayoyapita hayo hutoka kwa Mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini munaposema, museme tu: ‘Ndiyo,’ au ‘Hapana,’ kwa maana maneno yanayosemwa zaidi ya hayo yanatoka kwa yule mwovu Shetani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu.