Matthew 5:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninawaambia msishindane na yeyote anayetaka kuwadhuru. Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia shavu la pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi nawaambiani: Msibishane na mbaya! Lakini mtu akikupiga kofi shavu la kuume, mgeuzie la pili, alipige nalo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mimi ninawaambia: musirudishe mabaya kwa mabaya. Kama mutu akikupiga kofi kwa shavu la kuume, umugeuzie shavu la kushoto vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.