Matthew 5:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mnawapenda wale wanaowapenda ninyi, kwa nini mpate thawabu toka kwa Mungu? Hata watoza ushuru hufanya hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda ninyi? Hakuna! Kwa maana hata watoza ushuru hufanya hivyo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mkiwapenda wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi hayo hayo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mkiwapenda wanaowapendani mtapata mshahara gani? Je? Hata watoza kodi hawafanyi hivyo hivyo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zawadi gani mutapata kutoka kwa Mungu, kama mukiwapenda tu wenye kuwapenda? Hata walipishaji wa kodi wanaokuwa wakorofi wanatendeana vile!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?