Matthew 5:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu hawafanyi hivyo?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na ikiwa mnakuwa wema kwa rafiki zenu tu, ninyi si bora kuliko wengine. Hata watu wasiomjua Mungu ni wakarimu kwa rafiki zao pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu mnawapitaje wengine? Je? Hata wamizimu hawafanyi vivyo hivyo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama mukiwasalimia wandugu zenu tu, munatenda tendo gani la kupita wengine? Hata wapagani wanatendeana vile!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziyada? Hatta wattoza ushuru, je, nao hawafanyi kama hayo?