Matthew 6:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao kamilifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnapofunga, msijionyeshe kuwa na huzuni kama wanafiki wanavyofanya. Hukunja nyuso zao kwa kuonesha kuwa wana huzuni ili watu wawaone kuwa wamefunga. Ukweli ni kuwa wamekwishapata thawabu yao yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika, hao wamekwisha pata tuzo lao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mnapofunga msikunjamane nyuso kama wajanja! Kwani huzirembua nyuso, kusudi watu wawaone, wanavyofunga. Kweli nawaambiani: Wamekwisha upata mshahara wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Munapofunga kula chakula, musifanye kama wanafiki, wanaojigeuza kuwa wenye sikitiko na kukunja nyuso zao, kusudi watu waone kwamba wanafunga. Kweli ninawaambia: wamekwisha kupata faida yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.