Matthew 6:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo ninawaambia, msiyahangaikie mahitaji ya mwili; mtakula nini, mtakunywa nini au mtavaa nini. Uhai ni zaidi ya chakula na mavazi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nawaambiani: Msiyasumbukie maisha yenu mkisema: Tutakula nini? Tutakunywa nini? Wala msiisumbukie miili yenu mkisema: Tutavaa nini? Je? Maisha hayapiti vyakula? Nao mwili haupiti mavazi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ni kwa sababu hii ninawaambia ninyi: musijisumbue kwa ajili ya maisha yenu, kwa ajili ya chakula au kwa ajili ya kinywaji, wala musijisumbue kwa ajili ya miili yenu kwamba mutavaa nini. Uzima ni wa lazima kuliko vyakula, nao mwili ni wa lazima kuliko nguo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kiva sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni au mnyweni; wala mwili wenu, mvaeni. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?