Matthew 6:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waangalieni ndege wa mwituni: Hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao ndege?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waangalieni ndege wa angani. Hawapandi, hawavuni wala kutunza chakula ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, hamjui kuwa ninyi mna thamani zaidi ya ndege?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyoye. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waangalieni ndege wa mwituni: Hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watazameni ndege wa angani! Hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi waweke vichanjani. Naye Baba yenu wa mbinguni anawalisha nao. Je? Nyinyi hamwapiti hao?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie ndege wanaoruka katika anga: wao hawapandi mbegu wala hawavuni, wala hawaweki mavuno ndani ya gala, lakini Baba yenu anayekuwa mbinguni anawakulisha! Basi ninyi si wa lazima zaidi kuliko ndege wale?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Waangalieni ndege wa anga, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni awalisha hawo. Ninyi je! si bora kupita hawo?