Matthew 6:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hamwezi kujiongezea muda wa kuishi kwa kujisumbua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake au kuongeza dhiraa moja kwenye kimo chake?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwenu yuko nani anayeweza kwa kusumbuka kwake kujiongezea miaka yake kipande kama cha mkono mmoja tu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nani kati yenu, kwa ajili ya kujisumbua kwake, anaweza kujiongezea hata siku moja kupita muda wa maisha yake?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yupi katika ninyi awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja?