Matthew 6:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo unapowapa maskini, mtu yeyote asijue unachofanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata rafiki yako asijue ufanyalo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wewe ukimgawia mtu, mkono wako wa kushoto usitambue, wa kuume unayoyafanya,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wewe, unapomusaidia masikini, ufanye tendo lile kwa uficho hata rafiki yako wa kweli asijue.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali wewe utoapo sadaka, hatta mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume ufanyalo;