Matthew 6:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Kila siku ina masumbufu yake ya kutosha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msiisumbukie kesho. Kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Kila siku ina mahangaiko yake ya kutosha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, msisumbukie ya kesho! Kwani siku ya kesho itayasumbukia yaliyo yake. Inatosha, kila siku iwe na uovu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi musijisumbue kwa ajili ya kesho, kwa maana kesho itajisumbukia yenyewe. Kila siku ina masumbuko yake inayoitoshelea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi msisumbukie kesho; kwa kuwa kesho itayasumbukia mambo yake. Watosba kwa siku ubaya wake.