Matthew 7:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ijapokuwa ninyi watu ni waovu, lakini bado mnajua kuwapa vitu vyema watoto wenu. Hakika Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vyema wale wamwombao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama basi ninyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema wale wanaomwomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba yenu alioko mbinguni asizidi kuwapa mema wanaomwomba?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ikiwa ninyi munaokuwa waovu munajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, zaidi sana Baba yenu anayekuwa mbinguni atawapa wale wanaomwomba vitu vizuri zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao?