Matthew 7:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini lango la kuelekea katika uzima wa kweli ni jembamba. Na njia iendayo huko ni ngumu kuifuata. Na ni watu wachache wanaoiona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini njia inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena uko mlango ulio mfinyu, nayo njia yake inasonga; ndiyo inayokwenda penye uzima, lakini wanaoiona ni wachache.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini njia inayoongoza kufikia kwenye uzima ni yenye kusongamana na mulango unaoiingilia ni mwembamba, nao watu wanaoifuata ni wachache tu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali njia ni nyembamba iendayo hatta uzima, na mlango wake ni mwembamba: nao waionao ni wachache.