Matthew 7:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ewe mnafiki! Ondoa kwanza kipande cha mti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaweza kuona vizuri na kutoa vumbi katika jicho la rafiki yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ewe mnafiki, toa kwanza boriti kwenye jicho lako mwenyewe, nawe ndipo utakapoona wazi ili kuondoa kibanzi kilichoko kwenye jicho la ndugu yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mjanja, kwanza litoe gogo katika jicho lako! Kisha utazame vema, ndivyo upate kukitoa kibanzi katika jicho la ndugu yako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe munafiki, ondosha kwanza nguzo kutoka ndani ya jicho lako, kisha utaweza kuona waziwazi na kuweza kuondoa ile vumbi inayokuwa ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.