Matthew 7:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, yeyote anayeendelea kuomba atapokea. Yeyote anayeendelea kutafuta atapata. Na yeyote anayeendelea kubisha atafunguliwa mlango.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye hufunguliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye hufunguliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango hufunguliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kila mutu anayeomba, anapewa; naye anayetafuta, anapata, naye anayepiga hodi, anafunguliwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maaua killa aombae hupokea; nae atafutae huona, nae abishae alafunguliwa.