Matthew 8:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilipofika jioni, watu wengi waliokaliwa na mashetani waliletwa kwa Yesu. Naye aliyaamuru mashetani hayo kuwaacha watu. Na aliowaponya wagonjwa wote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuponya wagonjwa wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa wagonjwa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa jioni, wakampelekea wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno tu. Nao wote waliokuwa hawawezi akawaponya,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ilipokuwa magaribi, wakamuletea Yesu watu wengi waliokuwa na pepo. Naye akawafukuza wale pepo akiwaamuru kwa neno tu na kuwaponyesha wagonjwa wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,