Matthew 8:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameuchukua udhaifu wetu, ameyabeba magonjwa yetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yalifanyika ili litimie neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya, kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na akachukua magonjwa yetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ilitokea ili kutimiza maneno yaliyosemwa na nabii Isaya aliposema: “Aliyaondoa magonjwa yetu na kuyabeba madhaifu yetu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameuchukua udhaifu wetu, ameyabeba magonjwa yetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua magonjwa yetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua magonjwa yetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: “Yeye mwenyewe ameuchukua udhaifu wetu, ameyabeba magonjwa yetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kusudi litimizwe lililosemwa na mfumbuaji Yesaya: Yeye ameyachukua manyonge yetu, akajitwisha maumivu yetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifanya hivi kusudi yatimie maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Isaya: “Yeye alitwaa uzaifu wetu, naye amebeba muzigo wa magonjwa yetu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe alitwaa magonjwa yetu, na kuchukua maradhi zetu.