Matthew 8:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu lakini alikuwa amelala usingizi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula, kukatokea dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Isa alikuwa amelala usingizi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya mashua kutoka pwani, upepo wenye nguvu sana ukaanza kuvuma ziwani. Mawimbi yakaifunika mashua. Lakini Yesu alikuwa amelala.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu lakini alikuwa amelala usingizi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula kukainuka dhoruba kali baharini hata chombo kikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Isa alikuwa amelala usingizi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata mashua ikafunikwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu lakini alikuwa amelala usingizi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara kukawa na msukosuko mkubwa baharini, hata chombo kilifunikizwa na mawimbi, lakini yeye alikuwa amelala usingizi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja zoruba kubwa ikatokea katika ziwa na maji yakajitupatupa ndani ya chombo. Lakini Yesu alikuwa amelala usingizi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kukawa msukosuko mkuu baharini, hatta chombo kikafunikizwa na mawimbi: nae alikuwa amelala.