Matthew 8:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ngambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alifika ng'ambo ya ziwa katika nchi walimoishi Wagadarini. Hapo wanaume wawili waliokuwa na mashetani ndani yao na kuishi makaburini walimwijia Yesu. Watu hao walikuwa hatari sana na watu hawakuitumia njia iliyopita karibu na makaburi yale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi, ng'ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita katika njia hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ng'ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipofika ng'ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu wakitoka makaburini walikutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagadara, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wakitoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alifika katika nchi ya Wagadara, ngambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita njia hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika ng'ambo katika nchi ya Wagadara, watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitoka penye makaburi, ni wakorofi mno; kwa hiyo mtu hakuweza kuipita njia ile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipofika ngambo ingine ya ziwa la Galilaya, katika inchi ya Wagedari, watu wawili wenye pepo wakamufikia, wakitoka kwenye makaburi. Watu wale walikuwa na pepo wakali sana, hata hakuna mutu aliyesubutu kupita katika njia ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile.