Matthew 8:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa majini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo akawaamuru na akasema, “Nendeni!” Wale mashetani wakatoka ndani ya wale watu na kuwaingia nguruwe. Kisha kundi lote la nguruwe likaporomoka ziwani na nguruwe wote wakazama na kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa majini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likatelemka mbio gengeni, likaingia baharini na kufa ndani ya maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakateremka kwa kasi gengeni hadi baharini, wakafa maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia, “Haya, nendeni.” Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa majini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipowaambia: Haya! Nendeni! ndipo, pepo walipowatoka, wakawaingia nguruwe. Mara kundi lote likatelemka mbio mwambani, wakaingia baharini, wakafa majini;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na Yesu akawaambia: “Mwende!” Basi wakatoka ndani ya wale watu na kuingia ndani ya nguruwe. Mara moja kundi zima likatelemuka mbio toka kwenye maporomoko ya mulima na kujitupa ndani ya ziwa nao wakazama ndani ya maji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia. Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika kundi la nguruwe: na, kumbe! kundi lote la nguruwe likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini, wakafa majini.