Matthew 8:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wachungaji waliokuwa wakiwachunga wale nguruwe wakakimbia. Wakaenda mjini na kuwaambia watu kila kitu kilichotukia, hasa juu ya wanaume wale wawili waliokuwa na mashetani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote kuhusu yale yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote kuhusu yale yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayatangaza yote, hata mambo ya wenye pepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wachungaji wa nguruwe wale wakaenda mbio katika muji kupasha habari za mambo yaliyotendeka na habari ya wale watu wawili waliokuwa na pepo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia.