Matthew 8:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Isa. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha watu wote mjini walikwenda kumwona Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke katika eneo lao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Isa. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke katika nchi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara watu wa mji wakatoka wote, wakutane na Yesu. Walipomwona wakambembeleza, atoke mipakani kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi watu wote wa muji wakatoka kwa kumufikia Yesu na wakati walipomwona wakamusihi aondoke katika inchi yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; walipomwona, wakamsihi aondoke mipakani mwao.