Matthew 8:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajioneshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akamwambia, “Usimwambie mtu yeyote kilichotokea, lakini nenda kwa kuhani akakuchunguze. Na umtolee Mungu sadaka ambazo Musa aliamuru watu wanaoponywa watoe, ili iwe ushahidi kwa watu kwamba umepona.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu akamwambia, “Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu ye yote. Lakini nenda, ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Mose, iwe ushuhuda kwao kwamba umepona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila nenda zako, ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akamwambia: Tazama, usimwambie mtu! Ila uende, ujionyeshe kwa mtambikaji, ukitoe kipaji, Mose alichokiagiza, kije kinishuhudie kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akamwambia: “Angalisho, usimwambie mutu neno juu ya hii. Lakini kwenda na kumwonyesha kuhani jinsi unavyokuwa sasa. Kisha utoe sadaka kama Musa alivyoamuru, kuwa ushuhuda kwa watu wote kwamba umetakaswa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.