Matthew 9:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma, wala si tambiko.’ Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nendeni mkajifunze andiko hili linamaanisha nini: ‘Sihitaji dhabihu ya mnyama; Ninataka ninyi mwoneshe wema kwa watu.’ Sikuja kuwaalika wema kujiunga nami, bali wenye dhambi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma, wala si tambiko.’ Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma, wala si tambiko.’ Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nendeni zenu, mkajifunze maana ya neno hili: Huruma ndizo, nizitakazo, lakini vipaji vya tambiko sivyo. Kwani sikujia kuwaita wongofu, ila wakosaji.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muende kujifunza maana ya Maandiko Matakatifu yanayosema: ‘Ninataka huruma, lakini si sadaka zenu.’ Kwa maana sikukuja kuwaita wenye haki kunifuata, lakini watenda mabaya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.