Matthew 9:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha wanafunzi wa Yohane Mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wa Yahya wakaja na kumuuliza Isa, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha wafuasi wa Yohana wakamjia Yesu na kusema, “Sisi na Mafarisayo tunafunga mara kwa mara, lakini wafuasi wako hawafungi. Kwa nini?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha wanafunzi wa Yohane Mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakaja na kumwuliza Yesu, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wa Yahya wakaja na kumuuliza Isa, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo tunafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha wanafunzi wa Yohane Mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, “Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipomjia wanafunzi wa Yohana wakisema: Kwa nini sisi na Mafariseo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wa Yoane Mubatizaji wakamufikia Yesu na kumwuliza: “Sababu gani sisi na Wafarisayo tunafunga kula chakula, lakini wanafunzi wako hawafungi?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakati ule wanafunzi wa Yohana wakamwendea, wakinena, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga marra nyingi, bali wanafunzi wako hawafungi?