Matthew 9:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La, hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wanawezaje kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Kwenye harusi marafiki wa bwana harusi hawana huzuni anapokuwa pamoja nao, hivyo hawawezi kufunga. Lakini wakati unakuja ambao bwana harusi ataondolewa kwao. Ndipo watakuwa na huzuni kisha watafunga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La, hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Je, wageni wa bwana arusi waweza kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao, hapo ndipo watakapofunga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia, Walioalikwa harusini wawezaje kuomboleza, muda bwana harusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana harusi; ndipo watakapofunga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawajibu, “Je, walioalikwa harusini hutakiwa kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La, hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akawaambia: Walioalikwa arusini hawawezi kusikitika hapo, bwana arusi akingali pamoja nao. Lakini siku zitakuja, watakapoondolewa bwana arusi; ndipo, watakapofunga. Hakuna mtu anayetia kiraka cha nguo mpya katika kanzu chakavu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawajibu: “Munafikiri kwamba warafiki za bwana-arusi wanaweza kufanya kilio wakati bwana-arusi angali pamoja nao? Hapana! Lakini kutakuwa siku bwana-arusi atakapoondoshwa kati yao; ni siku zile watafunga kula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kuomboleza, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Lakini siku zitakuja atakapoondolewa bwana arusi; udipo watakapofunga.