Matthew 9:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu hawatii kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo iliyochakaa, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo, nayo hiyo nguo itachanika zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu anaposhona kiraka kwenye vazi la zamani, atatumia kiraka chakavu. Akitumia kiraka kipya vazi lake litachanika kwa sababu ya kusinyaa kwa kiraka hicho kipya. Kisha tundu litakuwa baya zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu hawatii kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo kuukuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo na kuchanika kwa nguo hiyo kutakuwa kubaya zaidi ya hapo mwanzo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo iliyochakaa, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo, nayo hiyo nguo itachanika zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu hawatii kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani kinaondoa pote paliposhonwa katika kanzu, hivyo tundu lake litakuwa kubwa zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hakuna mutu anayeshonea kiraka kipya juu ya nguo ya zamani. Kama anafanya vile, kile kiraka kipya kinapasua nguo ya zamani, na kupasuka kwake kunaongezeka zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hakuna mtu atiae kipande cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, likazidi kutatuka.