Matthew 9:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila, watu huweka divai mpya katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, watu hawawaweki divai mpya kwenye viriba vya zamani. Wakifanya hivyo viriba vitapasuka, na divai itamwagika na viriba vitaharibika. Daima watu huweka divai mpya katika viriba vipya, ambavyo haviwezi kupasuka, na divai huwa salama.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila, watu huweka divai mpya katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Navyo viriba vitaharibika, lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya na hivyo divai na viriba huwa salama.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila, watu huweka divai mpya katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala watu hawatii mvinyo mpya katika viriba vichakavu; kwani wakiitia mle, viriba vitapasuka, mvinyo imwagike, navyo viriba vitaangamia. Ila hutia mvinyo mpya katika viriba vipya; hivyo vyote viwili vitakaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile hawatii divai mupya ndani ya machupa ya ngozi yenye kuzeeka. Wakifanya vile yale machupa yanapasuka, halafu divai inamwangika, nayo machupa yanapotea bure. Lakini inafaa kutia divai mupya ndani ya machupa mapya ya ngozi, navyo vyote vinalindwa vizuri.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa watia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika: bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.