Matthew 9:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, kiongozi wa sinagogi akaingia, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipokuwa bado anaongea, kiongozi wa sinagogi akamwendea. Kiongozi akainama chini mbele yake na akasema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini ikiwa utakuja na kumgusa kwa mkono wako, atafufuka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yesu akiwa anawaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi, lakini uje uweke mkono wako juu yake naye atakuwa hai.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja kiongozi mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali twende umwekee mkono wako naye ataishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Alipokuwa akiwaambia haya, mara akaja jumbe, akamwangukia akisema: Binti yangu amekufa sasa hivi; lakini uje umbandikie mkono wako! mdipo atakapokuwa mzima tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa hajamaliza kusema maneno hayo, mukubwa mumoja akafika, akapiga magoti mbele yake na kumwambia: “Binti yangu anakufa sasa hivi; lakini kuja, uweke mikono yako juu yake kusudi apate kufufuka.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona.